Klabu ya Manchester United usiku wa kuamkia Leo Alhamisi imepoteza
mchezo wake wa kwanza wa EPL dhidi ya Spurs ikiwa na mshambuliaji wake
mpya Alexis Sanchez aliyehama kutoka Arsenal.
Man united wamekubali kipigo cha goli 2-0, magoli yaliyofungwa na P.Jones goli la kujifunga na Eriksen.
Matokeo mengine Chelsea wamekubali kipigo cha goli 3-0 dhidi ya AFC Bournemouth wakiwa nyumba Stanford Bridge.
Magoli ya Bournemouth yamefungwa na Wilson, Ake na Stanislas.
Vinara wa ligi hiyo Manchester City wameendeleza ubabe kwa ushindi wa goli 3-1 dhidi West Brom Albion.
Kwa matokeo hayo ya Jana Man City wameongeza gepu la pointi 15 dhidi ya Man United waliopo nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL.
Social Plugin