Manaibu Waziri, Mhe. Antony Mavunde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, (wapili kushoto), na Mhe. Dotto Biteko, kutoka Wizara ya Madini, (wapili kulia), wakipatiwa maelezo na Mjiolojia Mkuu wa mgodi wa Al-Hilal Minerals Limited wa mjini Shinyanga, (aliyenyoosha mkono), wakati wa ziara ya kushtukiza ya viongozi hao ili kubaini kama mgodi huo unazingatia sheria katika kutekeelza majukumu yake, Ziara hiyo waliifanya Februari 27, 2018
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SHINYANGA
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, na mwenzake wa Madini Mhe. Dotto Biteko, Februari 27, 2018 wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye mgodi wa almasi wa Al-Hilal Mineral Ltd ulioko kilomita 60 kutoka mjini Shinyanga, ili kubaini
kama wamiliki wa mgodi huo wanatekeleza sheria za uendeshaji.
Wakati Mheshimiwa Mavunde alikuwa akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF),
ikiwa ni pamoja na jinsi mgodi huo unavyotekeleza Sheria ya ajira na mahusiano kazini, Mhe. Biteko yeye alikuwa akifuatilia kwa nini mgodi huo haujawasilisha wizarani mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na mpango wa
uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR).
Kwa upande wake Mhe. Mavunde alibaini kuwa Mgodi huo bado ulikuwa haujajisajili na Mfuko na badala yake uongozi ulipeleka michango siku moja kabla ya ziara ya Naibu waziri.
“Serikali inataka waajiri wazingatie sheria, na ninyi mmevunja sheria kwa kutojisajili, ingawa mmelipa michango yenu jana, ninachoweza kusema, agizo la serikali la kuwafikisha mahakamani waajiri ambao hawajajisajili nchi nzima liko pale pale, ni juu yenu kutekeleza hilo kabla hamjapelekwa mahakamani.”Alisema Mhe. Mavunde.
Ziara ya Naibu Waziri ni muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 26, 2018 jijini Mwanza ambapo aliagiza kufikishwa mahakamani waajiri watatu jijini Mwanza.
Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko.
“Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna
sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.
Naibu Waziri Mvunde, akiwasikiliza wafanyakazi wa mgodi wa almasi wa Al-Hilal Minerals Limited wa mjini Shinyanga.
Mhe.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (kushoto), akiwa na mwenzake wa Madini Mhe. Dotto Biteko, wakati akizungumza kwenye kikao cha pamoja baina ya uongozi wa mgodi huo kwenye ziara hiyo ya kushtukiza Februari 27, 2018
Mhe. Biteko, (kulia), akiwa na Mhe. Mavunde, wakati akizungumza katika kkikao cha pamoja na uongozi wa mgodi huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw.Anslem Peter, (kushoto) na Naibu Kamish Idara ya Kazi, Bi.Rehema Moyo.
Kutoka kushoto, Bw. Anslem Peter, Bi. Rehema Moyo, na Bi. Laura Kunenge
Mhe. Naibu Waziri akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo.
Mwanasheria wa WCF, Bw. Deo, (kushoto), Afisa Kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, na Bw. Anslem peter
Naibu Waziri Mvunde akizungumza na baadhi ya manesi wa hospitali ya Kolandoto.
Naibu Waziri, akiongozana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kolandoto, Dkt. Maganga Ngoi (katikati) na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, wakati akitoka hospitalini hapo baada ya ukaguzi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe.Josephine Matiro, (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (wakwanza kushoto), na Afisa Kazi Mkoa wa Shinyanga, wakimsikiliza Bw. Anslem Peter.
Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, akifafanua masuala yahusuyo Sheria ya ajira na mahusiano kazini, Kulia ni Bw. Anslem Peter.
Naibu Wazuiri Mavunde, akizungumza mbele ya viongozi wa Hospitali ya Kolandoto mjini Shinyanga.
Manaibu Waziri Biteko, na Mavunde wakitoka mgodi wa Al-Hilal baada ya ziara yao ya ghafla.
Mwanasheria wa WCF, Bw. Deo Ngoi, (kushoto), akimsimamia Afisa Mwajiri wa Hospitali ya Kolandoto kujaza fomu za kujisajili na Mfuko huo.