Wanawake nchini Ghana wameonywa kutotumia dawa za kujichubua ili kubadilisha ngozi ya watoto kuwa nyeupe wakati bado wako tumboni kwa kutahadharishwa kuwa dawa hizo haramu zinapelekea madhara ya uzazi ikiwemo viungo vya ndani vya mtoto kuharibika.
Mamlaka ya Vyakula na Dawa Ghana (FDA) imesema utumiaji ya vidonge hivyo vijulikanavyo kama 'Glutathione' ni hatari na kwamba umma ifahamu kuwa hamna dawa zilizoruhusiwa na FDA vya kuchubua ngozi ya mtoto aliye tumboni.
Inadaiwa kwamba vitendo vya matumizi ya vidonge hivyo vinashamiri nchini Ghana na kwa mujibu wa FDA imesema kuwa mara nyingi vidonge hivyo vimekuwa vinaingizwa kinyemera ndani ya mizigo kwa viwango vikubwa kupitia viwanja vya ndege.
Aidha Polisi na vikosi vya usalama nchini humo wamesema kuwa wanafanya kazi pamoja na kuwashika na kuwashtaki makampuni na watu binfsi watakaokuwa na vidonge hivyo ambavyo tayari vimeshapigwa marufuku.