Wakazi wa kijiji cha Suiyan huko Samburu nchini Kenya, wametishia kuwaua watoto wao ili kuwaokoa na kuteseka kwa kifo cha taratibu na mateso, kutokana na njaa.
Kwa mujibu wa muwakilishi wa wanawake kutoka eneo la Samburu, Maison Leshoomo, jamii hiyo ya wafugaji imekuwa ikipoteza mamia ya mifugo, ambayo ndiyo tegemeo la maisha yao, na kuitaka serikali na wafadhili kuwapa msaada wa chakula ili kuwaokoa wakazi hao wanaokabiliwa na njaa kutokana na ukame
“Familia nyingi zimeachwa hazina kitu kabisa, ndio maana baadhi ya wanaume wametishia kuua watoto wao kuliko kuwashuhudia wakiteseka na njaa na hawana kitu cha kuwapa kula”, amesema Leshoomo.
Kwa upande wakechifu wa kijiji cha Suiyan Karoli Leraul, amesema watu wenye silaha pia wamekuwa wakiwavamia na kuiba mifugo yao, na mwaka 2017 takriban mifugo 7,000 iliibiwa na watu hao.