Tupo katika mwaka 2018 Wanasayansi wanaendelea kuonesha kuwa Teknolojia inakuwa mtu wangu, kutoka Uingereza siku za hivi karibuni wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh, wameeleza kuwa yai la binadamu (mwanamke) linakuzwa katika maabara kwa mara ya kwanza duniani.
Wataalamu hao wanaeleza kuwa Teknolojia hii mpya itasaidia kuvumbua njia mpya za kuhifadhi uzazi wa watoto ambao wako kwenye matibabu ya magonjwa ya saratani na pia ni fursa ya kuchunguza jinsi yai la binadamu linavyokua jambo ambalo milele yote limekuwa siri kwa sayansi.
Inaelezwa kuna imechukua miaka mingi ya kufanyia kazi teknolojia hiyo na hata walipofikia bado haijaweza kuanza kutumika rasmi na kwamba wataalamu sasa wataweza kukuza yai la mwanamke hadi kukomaa kabisa likiwa nje ya ovari.