Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AGPAHI YAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE MUHEZA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto  akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya  kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy  machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa  akimpongeza na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara  baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita  na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

****
SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya Ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya  kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy  machine).

Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa 
juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa  mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa  sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika  ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji  wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua  mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa  wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya  Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao  katika vifaa tiba.

"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii 
ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu  katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema  Mwakyusa.

Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru 
shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza  atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza (Muheza DDH) ili ianze  kazi.

"Nalishukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia 
kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali  ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya  alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalumu ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate 
huduma hiyo.

(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com