Mtoto Mase Denis kutoka Kabwana wilayani Rorya mkoani Mara aliyedaiwa kunajisiwa na baba yake wa kufikia Machi 3, mwaka huu alifariki dunia wakati akiwa njiani kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufani Bugando jijini Mwanza juzi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, Henry Mwaibambe aliwaambia waandishi wa habari kuwa awali mtuhumiwa Denis Ondigo alishtakiwa kwa kunajisi lakini kutokana na kifo hicho amebadilishiwa kuwa shtaka la mauaji.
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo majira ya saa 6 mchana wa Machi 3 akiwa nyumbani kwake Kabwana baada ya mama wa mtoto kuwa amekwenda dukani kununua mahitaji ya nyumbani.
Kamanda huyo alisema Ondigo (26) mkazi wa Kabwana alifikishwa Mahakama ya Wilaya Tarime mkoani Mara kwa mara ya kwanza Machi 13.
Social Plugin