Maadhimisho ya wiki ya maji mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Mwagala kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga yakiwa na kauli mbiu ya “Hifadhi maji na mfumo wa kiikolojia kwa maendeleo ya jamii”.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya wiki ya maji huadhimishwa kitaifa kuanzia tarehe 16 hadi 22 Machi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Akitoa hotuba yake,Talaba aliziasa kamati zote za maji katika mkoa kuhakikisha zinasimamia miradi ya maji vizuri ili iweze kudumu kwa muda mrefu na iendelee kutoa huduma iliyokusudiwa.
“Viongozi wote wa ngazi mbalimbali nawaagiza kuzisimamia kamati hizi kwa mujibu wa sheria ili ziendelee kutoa huduma bora kwa wananchi,kamati ambazo hazifanyi kazi ipasavyo zipigeni chini”,aliongeza.
"Hakikisheni pesa zinazopatikana kwenye mradi wa maji zisitumike kwenye miradi mingine,na viongozi wa siasa msiingilie kamati hizi,acheni zifanye kazi,wahandisi wa maji hakikisheni mnapita kwenye kila kamati ili muone mambo yanayoendelea",alisema Talaba.
Alisema ni jukumu la kila mwananchi kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji na kutofanya shughuli zinazoweza kuathiri vyanzo vya maji hususani shughuli za kilimo na ufugaji.
Aidha Nyabaganga alisema mkoa unaendelea kutekeleza program ya maendeleo ya sekta ya maji ‘Water Sector Development Program – WSDP’ inayolenga kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 95 ya wananchi waishio mijini na asilimia 85 ya waishio vijijini wapate maji safi na salama.
Alieleza kuwa hadi kufikia Desemba 2017 mkoa wa Shinyanga umefikia asilimia 53.7 ya utoaji wa huduma ya maji kwa upande wa vijijini na asilimia 70.5 kwa upande wa mijini.
Kwa upande wake Mhandisi wa Maji Manispaa ya Shinyanga Injinia Mariam Majala alisema jumla ya wakazi wa 135,618 wanaoishi katika manispaa ya Shinyanga wanapata huduma ya maji safi na salama inayotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini (SHUWASA) ikiwa ni sawa na asilimia 73 ya wananchi waishio mjini na vijijini.
Alisema manispaa hiyo ina jumla ya miradi ya maji ya bomba 10,visima virefu 30,visima vifupi 209 na matanki 72 ya kuvunia maji ya mvua yanayotumika kwenye taasisi mbalimbali.
Hata hivyo alisema manispaa ya Shinyanga haina mtandao wa mabomba ya majitaka hivyo wanategemea kuwa na huduma za uondoaji majitaka baada ya Wizara ya Maji kupitia wafadhili kuwa na mradi wa ujenzi wa mtandao na miundombinu ya uondoaji majitaka.
Maadhimisho ya wiki ya maji mkoani Shinyanga yameenda sanjari na uwekaji jiwe la msingi katika ofisi ya watumiaji wa maji kijiji cha Mwagala iliyojengwa kwa jumla ya shilingi milioni 5.2 kwa mapato mradi wa maji.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kijiji cha Mwagala kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wadau wa maji waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya wiki ya maji mkoa wa Shinyanga.
Akina mama wakimsikiliza mgeni rasmi.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akikata utepe wakati wa kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya watumiaji wa maji kijiji cha Mwagala kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga iliyojengwa kwa jumla ya shilingi milioni 5.2 kwa mapato mradi wa maji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akikata utepe wakati wa kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya watumiaji wa maji kijiji cha Mwagala.
Maandishi yanavyosomeka baada ya Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya watumiaji wa maji kijiji cha Mwagala.
Muonekano wa ofisi ya watumiaji wa maji kijiji cha Mwagala.
Muonekano wa ofisi ya watumiaji wa maji kijiji cha Mwagala.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez akiishukuru serikali kwa kuendelea kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akielezea namna serikali inavyoendelea kutekeleza miradi ya maji katika manispaa hiyo.
Wanafunzi wa shule ya msingi 'Shinyanga Modern Academy' wakitoa burudani ya wimbo kuhusu maji.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwagala wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini (SHUWASA) ,Injinia Sylivester Mahole akitoa neno wakati wa maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA),Injinia Joel Rugemarila akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uzalishaji na Usambazaji Maji (KASHWAS),John Zengo akitoa neno wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji mkoa wa Shinyanga.
Mhandisi wa Maji Manispaa ya Shinyanga Injinia Mariam Majala akitoa taarifa kuhusu hali ya maji katika manispaa ya Shinyanga.
Mtunza hazina Kamati ya watumiaji maji katika kijiji cha Mwagala Uwezo Issa akisoma taarifa ya ujenzi wa ofisi yao.
Wakazi wa Mwagala wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji.
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji.
Wanafunzi wakiwa katika eneo la tukio
Diwani wa kata ya Ibadakuli Msabila Malale akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kijiji cha Mwagala kilichopo kwenye kata hiyo.
Maadhimisho ya wiki ya maji yakiendelea
Wadau wa maji wakifuatilia matukio
Maadhimisho ya wiki ya maji yakiendelea.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini (SHUWASA) ,Injinia Sylivester Mahole akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA),Injinia Joel Rugemarila.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwagala Ngasa Mgongo akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji yaliyofanyika kimkoa katika kijiji chake.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin