Afisa Mifugo wilayani Kiteto mkoani Manyara William Msuya amesimamishwa kazi kwa kosa la ubadhilifu wa fedha za umma, za project ya kupigia chapa mifugo.
Akitoa taarifa ya kusimamishwa kwake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto Tamim Kambona, amesema kwamba Msuya amehusika na upotevu wa pesa za serikali milioni 60 ambazo zilikuwa za mradi, baada ya kufanya ukaguzi.
Tamim Kambona ameendelea kwa kusema kwamba Afisa huyo alikuwa hatoi risiti kwa wafugaji ambao ng'ombe wao wamepigwa chapa huku wengine akiwapatia, na walimtaka kuwasislisha fedha hizo lakini hata kazini alikuwa ahudhurii.
“Nimempa siku 14 arejeshe fedha hizo mara moja tena aingize benki na kuniletea risiti hata kwenye vikao anatuma msaidizi, kwa sasa anakuja kazini kwa muda anaotaka, kama hatorejesha mimi nitamfikisha mahakamani,” amesema Kambona.
Kambona amesema kwamba ameendelea kwa kusema na kutahadaharisha kwamba hatosita kumchukulia hatua mtumishi yoyote atakayeonekana kuihujumu halmashauri, na kutoa onyo kwa watumishi wa idara hiyo ya mifugo kuwa bado kuna watumishi ambao wameshiriki
Social Plugin