Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BABU WA MIAKA 90 ADAIWA KUBAKA WANAFUNZI WATANO SHINYANGA


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mwanaume aliyejulikana kwa jina la Kachuka Malongo(90) tuhuma ya kubaka wanafunzi watano wa shule ya msingi Tinde kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule alisema wanafunzi hao walibakwa kwa nyakati tofauti na mtuhumiwa akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa.

Alisema Machi 21,2018 majira ya saa 2 na nusu asubuhi,mkazi wa Tinde aitwaye Amada Mganyizi alibaini kubakwa kwa wanafunzi hao.

Kamanda Haule alisema wanafunzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa wana umri wa miaka kati ya 8 hadi 12 wanaosoma katika shule ya msingi Tinde A na B.

Alikitaja chanzo cha tukio hilo kuwa ni tamaa ya mapenzi na kwamba tayari wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi.

Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Aidha alitoa rai kwa wananchi na wazazi kuwa makini na karibu kwa watoto wao ili kubaini mabadiliko ya watoto na kuweza kuchukua hatua za haraka huku akiwaonya watu wenye tabia hizo kuacha mara moja.

Na Kadama Malunde- Malunde1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com