Mahakama Kuu leo imetoa amri kwa serikali kuweza kupeleka majibu ya maombi yaliyofunguliwa na Mawakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Abdul Nondo kujibu kesi ya kutompeleka Mahakamani kwa zaidi ya siku 10 tangu kukamatwa kwake.
Amri hiyo imetolewa leo Jumatano Machi 21 ambapo Mahakama kuu mbele ya Jaji Sameji iliwataka DCI,IGP na AG kufika mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtka juu ya Nondo ambapo leo majibu ya maombi hayo yametakiwa yapelekwe Machi 26 na walalamikaji kupeleka majibu yao ya nyongeza yapelekwe Machi 27.
Aidha mahakama inatarajiwa kusikiliza maombi ya pande zote mbili 04/08/18 kutoa hatma ya Abdu Nondo.
Kwa upande mwengine kesi ya mwanafunzi huyo (Nondo) iliyosikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 26 Machi 2018 ambapo Hakimu atatoa uamuzi kwamba mshitakiwa apewe dhamana ama asipewe dhamana, mshitakiwa amerudishwa rumande.
Social Plugin