Kiongozi wa kuiba kwa kutumia mtandao duniani amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Hispania kwa kutuhumiwa kuiba Paundi milioni 870 ambayo ni sawa na Shilingi trilioni 2.49.
Mtu huyo anasemekana kuwa kiongozi wa kundi kubwa la wezi hao wa mtandao duniani ambao walikuwa wanaendesha kampeni za software za Carbanak na Colbat ambazo zilikuwa zinaibia mabenki.
Mamlaka zinaeleza kuwa kundi hilo lilianza mwaka 2013 na liliibia benki takribani 100 kwa wakati huo.
Pesa hizo ziliibwa kwa kupitia njia za benki za kuhamisha fedha ambazo zinatolewa moja kwa moja kwenye mashine za kutolea fedha (ATM).
Social Plugin