Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LOWASSA,SUMAYE WAONDOKA MAHAKAMANI KESI YA MBOWE NA WENZAKE

Wajumbe wa kamati kuu CHADEMA ambao waliwahi kuwa Mawaziri wakuu wa Tanzania, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa, wameondoka katika mahakama ya Kisutu kabla viongozi wa CHADEMA hawajafikishwa mahakamni hapo.

Taarifa kutoka mahakama ya Kisutu zinasema kuwa kina Lowassa wameondoka eneo hilo huku wakitoa taarifa kuwa wanaelekea kwenye msiba wa mmoja wa wanachama wao.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa kina Mbowe Peter Kibatala, amesema kuwa Mbowe na wenzake watano hawajafikishwa mahakamani hapo mpaka sasa, kusomewa shtaka linalowakabili.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watano, hii leo wanatarajia kujua hatma ya dhamana yao juu ya kesi inayowakabili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com