Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu imekubali hoja 3 kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika kesi ya Babu Seya ikiwemo hoja ya Nguza Viking kutaka apimwe nguvu za kiume.
Akisoma hukumu kwa niaba ya majaji wenzake, Jaji Gerard Niyungeko aliainisha kwamba kati ya haki zilizokiukwa wakati wa mwenendo wa kesi hiyo ni ombi la Nguza Viking kupimwa kitabibu ili kuthibitisha kama hakuwa na nguvu za kiume na hivyo asingeweza kufanya vitendo vya ubakaji.
Mahakama hiyo imekubali pia hoja kwamba Viking (maarufu kama Babu Seya) na mwanaye, Johnson Nguza (maarufu kama Papii Kocha) hawakupata maelezo ya mashahidi wala fursa ya kuwahoji walotoa ushahidi ili kuthibitisha makosa.
Hata hivyo, hoja nyingine mbalimbali ziliwekwa kando ikiwemo hoja ya watuhumiwa hao kutolewa gerezani, huku mahakama ikisema kwamba tayari wameshatolewa kwa msamaha wa Rais John Magufuli.
Na Mussa Juma. Mwananchi
Social Plugin