Mbunge wa Arusha Mjini CHADEMA Mhe, Godbless Lema amefunguka na kuweka wazi kuwa kama chama cha siasa hakiwezi kufundisha watu wake kufanya siasa za kuleta fujo bali uvunjifu wa amani, uonevu ni vitu ambavyo vinaweza kuwafanya watu wapiganie haki zao.
Lema amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya CHADEMA na kusema kuwa wapo watu wengi ndani ya CHADEMA na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakilia na kuumia na mambo yanayoendelea nchini ndiyo maaana hata mwanaharakati Mange Kimambi kupitia mtandao wake wa kijamii amekuwa na nguvu kwa kuwa kuna watu ambao wanasikiliza kutokana na mambo yanayofanywa na serikali.
"Yaani msingi wa kwanza wa Demokrasia ni amani maanake watu washindane kwa hoja sasa inatosha maanake nini kumekuwepo na vilio vya CHADEMA na wanachama wake kwa muda mrefu sana bahati mbaya waandishi wa habari mkafikiri vilio hivi vya CHADEMA, kanisa likafikiri hivyo na msikiti ukafikiri hivyo lakini leo tunalia pamoja wakiwepo wafanyabiashara sasa leo kilio chetu si pekee yetu ndiyo maana kanisa limetoa waraka hivi karibuni Katoliki na Lutherani tunategemea BAKWATA watafanya hivyo hivyo sasa ipo siku na hiyo siku inakuja"
Lema aliendelea kusema kuwa "Kuna uchungu unakusanyika kwa watu na hawa watu wanaandamana moyoni ndiyo maana Mange Kimambi yuko Marekani anatumia Instagram huku anajibiwa na kiongozi, Mwigulu Nchemba, Mambosasa, sasa kama mtu mmoja yupo Marekani anaweza kuhamasisha Tanzania na kukawa na presure tunayoiona hii maanake kwamba watu wamechoka, tunasema imetosha lengo la CHADEMA au lengo langu mimi au lengo la kiongozi yoyote wa CHADEMA si kuona nchi hii haina amani lakini lengo la Chama Cha Mapinduzi kwa mwelekeo wao ni kuona watu wanaingia barabarani kwa nguvu kutafuta haki" alisema Lema.
Social Plugin