Mkurugenzi Mtendaji wa MSD Laurian Bwanakunu amesema baada ya kuongezewa bajeti yao kufikia bilioni 250 kwa sasa MSD wanasambaza dawa zenye thamani ya bilioni 18 na lengo ni kufikia bilioni 21 ikifika mwezi Julai.
Bwanakunu ameyasema hayo leo Jumatatu, Machi 26 katika hafla uzinduzi wa magari mapya 181 ya MSD kwa ajili ya kusambaza dawa na vifaa tiba.
Aidha amefafanua kwamba licha ya usambazaji huo wa dawa bado changamoto imekuwa katika makadirio ambapo kituo cha afya kinaweza kusema "wanahitaji makopo 20 ya panadol wakati mahitaji ni makopo 60, dawa zikiisha tunalaumiwa MSD."
Pamoja na hayo Mkurugenzi wake amepongeza na kushukuru kwa magari yaliyotolewa ambapo amkiri kwamba ni kiwango kikubwa kuwahi kupokelewa tangu kuanzishwa kwa MSD.
"Tangu MSD ianzishwe mwaka 1994 hatujawahi kupokea magari mengi kiasi hiki, gharama yake ni bilioni 20.7. Sasa tutakuwa na jumla ya magari ya kusambaza dawa na vifaa tiba 213, hii ni hatua kubwa sana katika kutanua wigo na uharaka wa kazi zetu,"amesema Bwanakunu.
Social Plugin