Utafiti uliofanyika kwa kuhusisha watu 5,177 umebaini waishio na nguvu kidogo za kiume wana uwezekano wa asilimia 20 kuugua maradhi kadhaa.
Baadhi ya maradhi hayo yanatajwa kuwa ni mafuta mengi mwilini, pia shinikizo la damu, huku wakiwa hatarini kuugua maradhi kama kisukari.
Kutokana na hilo, watafiti wana ushauri kwamba, mtu akibainika na nguvu kidogo za kiume anapaswa kukaguliwa afya yake katika maeneo mengine ya kiafya.
Mwanataaluma Profesa Alberto Ferlin, kutoka Chuo Kikuu cha Bresci, aliyeongoza utafiti huo anasisitiza:"Wanaume hao wako hatarini kupata matatizo mengine ya afya ambayo yanaingiza maishani yake hatarini.”
Mtaalamu Profesa Ferlin, anashauri kila anayekutwa na shida hiyo ya nguvu kidogo ya kiume, afya yake ifuatiliwe kwa karibu.
Mshauri Kevin McEleny kutoka, Uingereza anashauri kuwa katika hali iliyoko Uingereza, katika hali iliyozoeleka nchini Uingereza, watu wenye shida ya nguvu ya kiume hawafuatiliwi sana.
Chanzo- Nipashe
Social Plugin