NAIBU WAZIRI MAVUNDE AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 35 KIWANDA CHA NYUZI CHA PPTL TANGA KWA UKIUKWAJI WA SHERIA

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amekitoza faini ya shilingi milioni 35 (milioni thelathini na tano), kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko eneo la Kange Mkoani
Kilimanjaro.

Mhe.Mavunde alichukua uamuzi huo, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo Machi 2, 2018 ili kubaini waajiri ambao hawatekeelzi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

Naibu Waziri Mavunde, alikuta wafanyakazi wa kiwanda hicho ambacho kina mashine nyingi na kutokana na mfumo wa utendaji kazi wake, kinatoa kelele nyingi hawakuvaa vifaa vya kujikinga na madhara kazini, (protective gears).

Mhe. Mavunde aliwakuta baadhi yao wakiwa wamevaa kandambili, wengine hawana vifaa vya kuziba masikio kujihami na kelele, pamoja na vifaa vingine.

Hatua hiyo ilimkasirisha Mhe. Naibu Waziri na kumuagiza Afisa wa OSHA, kuchukua hatua mara moja ambapo kiwanda hicho kilitozwa faini ya shilingi milioni 35 kwa kukiuka Sheria ya ajira na mahusiano kazini ambapo pamoja na mambo mengine inasisitioza usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi kuvaa vifaa
vya kujihami.

Aidha Mhe. Mavunde ambaye kabla ya kufika Mkoani Tanga,
alitembelea mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kilimanjaro, ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuondoa kasoro hizo mara moja.

Sambamba na hilo, Mhe. Mavunde amesema, serikali haitabadili
msimamo wake wa kuwafikisha mahakamani waajiri wote ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) kwani kwa kutofanya hivyo wanakabiliwa na adhabu mbalimbali
ikiwemo kupelekwa mahakamani ambapo mwajiri atakayepatikana na hatia atalazimika kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi Milioni 50,000, (Milioni Hamsini), au kifungo kisichopungua miaka mitano (5) au vyote kwa pamoja.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao bado hawajajisajili na WCF na ambao hawafuati sheria ya ajira na mahusiano kazini, mkoani Tanga Ijumaa Machi 2, 2018, Mhe. Mavunde alisema.

“Si jambo zuri kwa waajiri kutekeleza matakwa hayo ya kisheria
hadi wanapoona kiongozi wa serikali amewafikia, hii siyo sawa, na kuonya kuwa ni muhimu waajiri wakatambua kuwa zama zimebadilika, hakuna kichaka cha kujificha, vichaka vyote vinawaka moto hivi sasa” ,alisema.

Mhe. Mavunde pia aliwatahadharisha waajiri ambao wamejisajili kwa kupeleka taarifa za uongo kuhusu shughuli zao ikiwa ni pamoja na idadi ya wafanyakazi wao na viwango vya malipo ya mishahara ya wafanyakazi hao, kwani kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai.

Naibu Waziri ambaye kwa sasa yuko katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Aira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama alilotoa mwishoni mwa mwaka jana, la kuwataka waajiri kutoka sekta rasmi (umma na
binafsi) Tanzania Bara, kutekeleza takwa la kisheria linalowataka kujisajili na kutoa michango Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

“Kama nilivyowaeleza wenzenu kwenye mikoa niliyotembelea ya
Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro na leo hapa Tanga ninarudia tena, nia ya serikali ni kuwaondolea mzigo wa gharama waajiri, ya kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakati wakitekeelza majukumu yao ya kikazi, na badala yake wajibu huo uchukuliwe na serikali kupitia Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi”.

Tunataka ninyi waajiri mjikite zaidi kwenye shughuli zenu za
msingi za kufanya biashara na uwekezaji, na jukumu la kuwahudumia wafanyakazi wanapodhurika kazini tuachieni sisi serikali, alisisitiza Mhe. Antony Mavunde.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, Mkoa wa Tanga una jumla ya waajiri 769 na kati ya hao, ni waajiri 413 tu ndio wamejisajili, huku wengine 356, bado hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili na kupeleka michango kwenye
Mfuko.

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018. 
Naibu Waziri akitembelea kiwanda hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,(watatu kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko Kange Mkoani Tanga, baada ya kuwakuta wakifanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya kujikinga, (protrctive gears), alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sharia ya kazi na mahusiano kazini sambamba na kuwabaini waajiri a,mbao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani humo Machi 2, 2018. 
Naibu Waziri Mavunde, akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, wakati walipotembelea kiwanda hicho cha PPTL.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (katikati), akizungumza na Mkuu wa Kituo cha Afya, Tumaini Health Centre kilichoko Chumbageni Mkoani Tanga, Sister Flora Mushi, (kulia), ambapo alibaini bado mwajiri huyo hajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuagiza afikishwe mahakamani kwa kosa hilo la jinai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter.
Naibu Waziri na ujumbe wake, wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe.Martin Shigela, (katikati), mwanzoni mwa ziara yake aliyoifanya mkoani humo Machi 2, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa, (kushoto), akizungumza na Naibu Waziri Mabunde, (watatu kulia), Bw. Anselim Peter, (wapili kulia) na Kamishna wa Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo.
Mhe. Mavunde, akiwa na Bw. Anselim Peter, wakati wa ukaguzi huo.

Mhe. Mavunde akisalimiana na Bi. Rehema Moyo.
Mhe. Mavunde akisalimiana na Bw. Anselim Peter (kulia).
Mhe. Mavunde akizungumza kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu, shule ya Sir John iliyoko Ras Kazoni Mkoani Tanga. Katikati ni Bw. Anselim Peter na Bi. Rehema Moyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post