Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilishia Wizara baadhi ya Mawaziri.
Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais; na shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.
Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:
- OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu
- OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman
- Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma Mwalim
- OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar Kheri
- Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis
- OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed
- Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga
- WIZARA YA AFYA
- Waziri wa Afya- Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed
- Naibu Waziri wa Afya – Mheshimiwa Harusi Said Suleiman
- WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI
- Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Salama Aboud Talib
- Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Juma Makungu Juma
- WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA
- Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Balozi Amina Salim Ali
- Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidh
- WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Riziki Pembe Juma
- Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri
- WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
- Waziri wa Fedha na Mipango – Mheshimiwa Dkt. Khalid Salum Mohamed
- WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE
- Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo
- Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Choum Kombo Khamis
- WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO
- Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Maudline Cyrus Castico
- Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Shadia Mohamed Suleiman
- WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI
- Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Rashid Ali Juma
- Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Dkt. Makame Ali Ussi
- WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI
- Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa Mamboya
- Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Mohamed Ahmada Salum
- WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
- Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Mheshimiwa Balozi Ali Abeid Karume
- Naibu Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Mheshimiwa Lulu Msham Abdulla
Aidha, Mheshimiwa Said Soud Said na Mheshimiwa Juma Ali Khatib wanaendelea kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum.