Mbunge
wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Nape
Nnauye amefunguka na kudai kutohusika na kupanga mambo mbali mbali
yanayoendelea nchini baada ya kutuhumiwa kufanya hilo na mmoja wa raia.
Nape
Nnauye amefunguka hayo wakati akijibu moja ya hoja ya mtu aliyemtuhumu
yeye kama Mbunge wa CCM na kusema kiongozi huyo anajua na kuona haki za
raia zikivurugwa
"Naamini
unaitwa Kusiluka,nimesoma lawama zako kwangu,una haki ya kulaumu ili
upumue, lakini kuna kikao nimeshiriki kupanga hayo unayonituhumu?!
Nadhani kuwa mkweli kwa nafsi yako tuhuma hizo ni nzito si sawa kuzisema
bila kuwa na hakika, sihusiki na hayo usemayo na nayalaani pia" Alidai
Nape Nnauye
Nape
Nnauye aliwataka Watanzania kwa pamoja kuwasha mishumaa ya matumaini na
hapo ndipo mtu huyo alipoibuka mwananchi huyo na kusema kuwa kiongozi
huyo yeye anatambua na kujua kinachoendelea nchini sasa, jambo ambalo Nape Nnauye amelikana na kusema hata yeye analaani kwa vitendo vinavyoendelea nchini.