Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limewakamata na kuwawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii yanayotarajiwa kufanyika April 26 mwaka huu.
Kamanda wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto amesema watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.
Aidha Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye atakamatwa atashughulikiwa kisheria
Mbali na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii.
Social Plugin