Rais
Joh Magufuli amewanyanyua Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za
Serikali(CAG), Profesa Mussa Assad na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Dotto James kueleza kama kuna upotevu wa Sh 1.5 trilioni kama
inavyodaiwa.
Rais
Magufuli aliwataka watendaji hao waeleze hilo leo Ijumaa Aprili 20,
Ikulu wakati akizungumza baada ya kumaliza kuwaapisha majaji wapya kumi
aliowateua hivi karibuni.
“Kuna
watu wanaposti posti vitu kwenye mitandao kwamba kuna upotevu wa
shilingi trilioni 1.5 mimi nimefuatilia hilo sijaona upotevu huo.
Niliposikia taarifa hizo nikampigia CAG mbona kwenye ripoti yako
uliyoniletea hapa Ikulu hukuonyesha hilo eneo la upotevu hilo akaniambia
hakuna... maana angeniambia tu siku ile ile hata kama ni waziri
ningemtimua,” amesema.
Baada ya kueleza hivyo, Rais Magufuli alianza kuwahoji watendaji hao akitaka wathibitishe kama kweli upotevu huo umetokea.
“Bahati
nzuri CAG yuko hapa... embu tuthibitishie kama fedha hizo kweli
zimepotea,” amesema Rais Magufuli kabla CAG kusimama na kujibu;
“mheshimiwa hapana... hakuna upotevu uliokuwepo.” Baada ya CAG kutoa
majibu hayo Rais Magufuli akamhoji Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango
asimame kujibu swali hilo hilo.
“
Hakuna upotevu huo mheshimiwa Rais...Hazina tuko salama,” alisema
Dotto. Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kutokuwepo kwa opotevu huo
huku akionyesha kusikitishwa namna watu wanavyotumia uhuru wa mitandao
kutuma yale wanayoyapenda.
“Kwa vile hii mitandao hatukontro sisi basi watu wanapostiposti vitu wavitakavyo hata kama siyo vya kweli,” amesema.
Social Plugin