Hofu imetanda kwa wakazi wa kijiji cha Kiambaa katika Jimbo la Embu Mashariki nchini Kenya baada ya mwanaume mmoja kumvamia na kumshambulia rafiki yake kwa mapanga hadi kufariki.
Tukio hili linaripotiwa kutokea jumapili ya April 8, 2018 usiku na baada ya mwanaume huyo kumuua mwenzie kwa mapanga naye alikwenda kujinyonga hadi kufa kwenye mti wa maparachichi.
Dancan Muriuki Nyaga, 31, ambaye ndiye alimuua rafiki yake Nyaga Murunguru kisha kujinyonga anaripotiwa kuwahi kuapa mbele ya watu kwamba kuna siku ataua mtu na baadaye atajinyonga.
Social Plugin