ASKOFU KAKOBE: 'WAMECHUKUA PASSPORT YANGU..KAMA SIYO RAIA,NIAMBIE MIMI RAIA WA NCHI GANI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amefunguka baada ya kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani katika Idara ya Uhamiaji na kusema kuwa watu hao wamemuhoji kuhusu uraia wake na kudai kuwa wamechukua passport yake. 

Mchungaji Kakobe amedai kuwa watu hao hata kipindi cha nyuma walishakwenda kuchunguza juu ya uraia wake kwa kuwauliza ndugu na jamaa mbalimbali na kujiridhisha kuwa yeye ni raia wa Tanzania hivyo anadai anashangwaza kuona akiitwa sasa tena kwa ajili ya suala la uraia. 

"Mimi nilijiunga na jeshi la kujenga taifa mwaka 1974 mpaka sasa ni miaka 44 nimeenda kuwa trained kama mwanajeshi maana yake hiyo, miaka 44 imepita leo sasa ndiyo wananza kuzungumza masuala ya uraia unaona kabisa kuna shida, hivyo ni rahisi mtu kudhani kuna jambo, kwanini sasa? 

" Pamoja na kazi nzuri hii ambayo ni kazi yao na kawaida yao lakini ni rahisi kuhisi kitu kingine. Sasa hivi wamechukua passport yangu na wamesema sababu ya kuchukua passport hiyo ni kwamba kule itakuwa rahisi kupata taarifa za 'Afidavit', ambazo zinatakiwa kwenye maelezo. 

"Na nimetoa taarifa za passport zangu nne kwa sababu nimekuwa na passport nne katika kipindi chote na nimetoa kila kitu kuhusu passport hizo" alisema Kakobe 

Kakobe aliendelea kusema kuwa maafisa hao wa uhamiaji wamemwambia kitendo hicho kinaweza kuwa cha siku moja au mbili hivyo kwa sasa hawezi kusafiri nje ya nchi ya Tanzania mpaka atakapokabidhiwa tena passport hiyo. 

Aidha Kakobe amesema kitendo cha yeye kuhojiwa kuhusu uraia wake kama umepelekewa na baadhi ya mambo ambayo yametokea huko nyuma hivyo kutumia njia hiyo kama fimbo amedai inapoteza maana.

"Umemtaja Nondo, umemtaja Askofu Niwemugizi mimi mwenyewe utaona 'line' zote zinafanana, ningetarajia kwamba liwe zoezi la watu wote ili kucheki na kuthibitisha ingeeleweka zaidi lakini fulani, fulani, fulani, ndiyo maana mimi nasema mwenye haki ni jasiri kama Simba maanake kama hakuna uovu wala chochote kilichofichika mimi huwezi kuniambia siyo raia wa hapa, ukianiambia siyo raia wa hapa itabidi uniambie raia wa nchi gani na itabidi uthibitishe kama mimi ni raia wa kule" alisisitiza Kakobe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post