Ikiwa leo April 19, 2018 msanii Alikiba ameoa, mshindani wake kimuziki Diamond Platnumz hajakaa kimya kwenye hilo.
Diamond amefunguka kuwa amepewa taarifa za Alikiba kuoa siku , hivyo amemtumia salamu na kumtakia maisha mema ya ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram tumekuletea kile alichogusia kuhusiana na ndoa ya Alikiba;
"Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 " ameandika Diamond.
Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake Aminah Rekish mjini Mombasa nchini Kenya.
Social Plugin