Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Lawyers Society – TLS), akichukua mikoba ya aliyekuwa Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu baada ya muda wake kumalizika.
Katika uchaguzi huo, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.
Aidha, Ndugu Omar Shaaban amechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar Lawyers Society.
Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho, Uongozi wa TLS hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, na baada ya hapo viongozi wengine huchaguliwa.
Social Plugin