Msemaji wa timu ya soka ya Simba Haji Sunday manara, amefunguka kuhusu umaarufu wa msanii wa filamu bongo Wema Sepetu,na kusema kwamba msichana huyo ni mrembo haswa lakini hajaweza kutumia umaarufu wake kutengeneza pesa.
Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Manara amesema anaamini Wema ni miongoni mwa wanawake wachache sana Tanzania ambao ni maarufu na warembo ambao wanaweza kusimamisha nchi, lakini hajatumia kipawa alichopewa, hivyo kwake ni sawa na bure.
“Wema ni msichana mzuri, mrembo, ni katika wasichana wenye nguvu sana na ushawishi Tanzania, ni mwanamke maarufu katika 'top 3' ya wanawake maarufu zaidi, anaweza akatumika hata katika matukio makubwa ya nchi, ni bado tu labda hajaweza kutumia hivyo vipawa Mungu alivyompa, kufikia mafanikio ya juu kabisa, naamini mwanadamu ukiwa maarufu wa kiwango kama cha Wema lazima uwe na kisu cha kufa mtu, sitaki umaarufu takataka halafu unakuwa mzigo huna”, amesema Manara .
Manara ameendelea kwa kusema kwamba anamshauri msanii huyo kutumia fursa ya umaarufu alionao kutengeneza pesa, kwani kipawa alichopewa cha kukubalika na kupendwa ni kikubwa zaidi.
Social Plugin