Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Vincent Mashinji amesema sharti la kuripoti kituo Kikuu cha Polisi Central ni gumu kulingana na kazi wanazozifanya.
Dr. Mashinji ameyasema hayo leo April 20, 2018 baada ya yeye na Viongozi wenzake wa chama hicho kuripoti kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya sharti la dhamana walilopewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Dr. Mashinji amesema, “Iliamuriwa na mahakama kila siku ya Ijumaa turipoti kwa RPC hapa Central Polisi ikiwa kama sehemu ya sharti la dhamana tulilopewa mahakamani kwenye ile kesi yetu inayojumuisha watu 9”
“Kimsingi ukiangalia ni sharti gumu kwani nature ya kazi zetu inatutaka kusafiri kwenda kujenga chama, hivyo tunashindwa ila kwa vile ni amri ya mahakama lazima tutekeleze kwani ndio inatenda haki,” -Dr. Mashinji.
Pia Dr. Mashinji amesema kama mahakama itaridhia kuwaondolea sharti hilo itawasaidia sana.
Social Plugin