Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAULI YA STAA ZA MUZIKI BONGO ALIKIBA BAADA YA KUFUNGA NDOA LEO


Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya.

Harusi hiyo ya kukata na shoka iliofanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum ilihudhuriwa na rafiki wa mwanamuziki huyo Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Mwanamuziki huyo wa wimbo wa Seduce me aliisafirisha familia yake mjini Mombasa siku moja kabla ya kumuoa mchumba wake.

Ni watu wachache pekee walioalikwa katika harusi hiyo iliodaiwa kufanyika kisiri.


Baada ya kufunga ndoa staa huyo wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba‘ amefunguka na kusema kwamba, yeye alinusa tu na akajikuta amempenda binti mrembo Amina Khaleef kutoka Mombasa ambaye leo, Aprili 19, 2018, amefunga naye pingu za maisha.

“Wanasemaga macho hayana pazia na moyo hauna macho, lakini mimi moyo wangu umenusa tu mpaka huku, sijaweza kuona lakini moyo wenyewe ndiyo umependa, nipo Tanzania, ningeonaje huku Kenya? Moyo ndiyo umependa

“Nimejiona nimetimiza umri, ni wakati wangu kuwa na mke, maisha ndiyo haya haya kinachotakiwa ni kupigana nayo ili uweze kuishi vizuri,” alisema Kiba.


Kiba na Amina wamefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa leo Asubuhi ambapo tukio hilo limeshuhudiwa pia na ndugu na marafiki zake wa karibu.

Aidha, Kiba amesema ameamua kufunga ndoa yake siku ya leo kwani siku kama hii ndiyo wazazi wake walifunga ndoa yao miaka kadhaa iliyopita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com