Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJAJI WAWILI WAJIUZULU BILA KUTAJA SABABU

Majaji wawili wa Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamejiuzulu kwenye nafasi zao, na kusalia majaji sita badala ya tisa katika Mahakama hiyo.

Jaji mmoja alifariki dunia siku ya Jumapili na wengine wawili wamejiuzulu bila hata kutoa maelezo au sababu ya kujiuzulu kwao.

Majaji hao ambao ni Jean-Louis Esambo na Banyaku Luape wamedaiwa kutoripoti katika Mahakama ya Katiba, Mnamo Oktoba 17, 2016, ambayo ingetoa uamuzi muhimu kuhusu hatma ya DRC.

Imeelezwa kwamba Tangazo hilo limeishangaza serikali ya DRC kwa uamuzi huo ingawa majaji hao wawili walionesha zaidi ya mara moja maoni tofauti na rais wa mahakama hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com