Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni raia wa Afrika Kusini, amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kosa la kumlinda mbakaji wa mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili, na mahakama kuu ya Johanesburg.
Mwanamke huyo ambaye hajatajwa jina kwa ajili ya kulinda utambulisho wa mtoto wake, alikuwa akikanusha taarifa ya daktari na kile kilichoaminiwa na mahakama baada ya mtoto wake wa miezi miwili kuonekana amebakwa na kuumizwa vibaya.
Mama huyo amekuwa akisema mtoto wake hajabakwa isipokuwa ameanguka wakati akiwa amelala na kuangukia goti lake, na ndipo alipoumia.
Lakini hata hivyo mahakama ilimbana mwanamke huyo kwa kumuuliza kama alinguka na hakubakwa majeraha ya ndani na mbegu za kiume alizitoa wapi, na kushindwa kujibu huku akisisitiza hajabakwa na mtu yeyote.
“Mtuhumiwa anashindwa kuelezea ni kwa namna gani mtoto ameumia kwa ndani na sio nje, na ushahidi unaonyesha sehemu za kiume ziliingia ndani ya sehemu za siri za mtoto na kumjeruhi (kumpasua), namna pekee ambayo tunaweza kujua ni namna gani ilitokea, ni yeye pekee ndiye anayejua”alisikika Jaji Veenendal Said.
Mahakama ya Afrika Kusini ilikuwa inamtaka mama huyo kumtaja mtu aliyemfanyia kitendo hiko cha ukatili mtoto huyo ambaye memzaa mwenyewe, na kueleza kilichotokea, lakini mwanamke huyo kukataa kata kata, na mahakama kushwangazwa ni kwa nini hataki kusema ukweli na kumhukumu kwenda jela maisha.
Taarifa zinasema kwamba mwanamke huyo ameolewa na amekuwa akiishi kwenye ndoa yenye manyanyaso na vipigo kutoka kwa mume wake, na hata alipokuwa kwenye kesi mume wake huyo hakuja kumtembelea wala kumletea mahitaji yoyote ya msingi, tangu Novemba 2016 ambapo tukio hilo la ubakaji lilitokea.
Social Plugin