Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe jana April 17 amezuiwa na maafisa wa jeshi la polisi kuongea na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani katika kesi yao inayowakabili ya kufanya maandamano yaliyopelekea kifo cha Akwelina.
Baada ya Mbowe na viongozi wengine waandamizi wa CHADEMA kutoka mahakamani waandishi wa habari walijotokeza na kutaka kufahamu kilichojiri na kupata maelezo yoyote kutoka kwa viongozi hao lakini alijitokea afisa mmoja wa jeshi la polisi na kuwazuia viongozi hao wasifanye mazungumzo na waandishi wa habari katika viunga hivyo vya mahakama kwa kudai kuwa hawapaswi kufanya hivyo.
Jambo hilo lilileta mvutano wa maneno katika ya viongozi hao wa CHADEMA pamoja na Afisa huyo wa polisi, lakini baadae Mwenyekiti wa CHADEMA aliaanza kuondoka akielekea kwenye gari yake hapo ndipo alitumia nafasi hiyo kuwaeleza waandishi wa habari kuwa jeshi la polisi halitaki wao waongee na waandishi pamoja na Umma kiujumla.
"Tunapotoka lazima tutoe statement kwa vyombo vya habari sasa unataka tukafanyie barabarani au tukatafute ukumbi, nyinyi mna abuse power ambayo unapewa na state, yaani mnapitiliza . Jamani inabidi tuachie hapo tu maana mnaona wamekataa tusizungumze na sisi hatutazungumza lakini haki itabakia haki, hatujawahi kuona watanzania wanazuiwa kuzungumza na watanzania wenzao kuwapasha habari. Walitukamata na kutuleta kwenye mashtaka hiyo yenyewe ni habari saizi wanakataza hata tusizungumze hili jambo la ajabu sana ni matumizi mabaya ya madaraka na polisi wakiendelea na mtindo huu wataleta vurugu zisizo na sababu katika nchi ahsanteni sana" alisisitiza Mbowe
Social Plugin