Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema hajasita kuweka wazi hisia zake baada ya kutambulishwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika Ibada ya kusimikwa Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha.
Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter ameonekana kushangaa kitendo cha RC Gambo kumuita yeye rafiki.
Ameandika; “Katika Ibada ya kusimikwa Askofu, Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki. Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena. Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana. Mrisho Gambo(RC) yeye hakuogopa kuwa muongo madhabahuni, eti aliniita Mimi rafiki yake."
Social Plugin