Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amevitaka vyombo vya dola kuwashughulia watu wanaodaiwa kuwa wakorofi hasa wanasiasa, kwa kuwaweka ndani ili kurekebisha tabia zao.
Msukuma alitoa wito huo juzi Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na Sheria.
“Sisi kama wabunge tunaotunga sheria tuviachie vyombo vifanye kazi yake, wanaosema kuna watu wamepotea hata watu wa CCM wamepotea wengi tu, wamechinjwa Kibiti wengi tu na hatukupiga kelele tumeviachia vyombo vinalishughulikia.
"Hata mimi nilifanya kosa na niliwekwa ndani. Hawa wakorofi wakifanya makosa wawekwe magereza, unamuona Lema sasa hivi kidogo amekuwa binadamu,” alisema.
Aidha, Msukuma alimuomba Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kupeleka bungeni muswada wa kubadilisha sheria ili makosa yasiyo stahili mtuhumiwa kufungwa apewe adhabu ndogo ili kuondoa msongamano wa wafungwa magerezani.
Social Plugin