Mbunge wa Ileje (CCM) Janeth Mbene amepiga magoti bungeni na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kupeleka maendeleo kwenye wilaya yake anayodai ilisahaulika.
Mbene amefanya kitendo hicho leo bungeni Aprili 13,2018 wakati akichangia bajeti ya ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Mara baada ya kuruhusiwa kuchangia bajeti hiyo, Mbene amesema wilaya ya Ileje ni ya miaka mingi lakini ilikuwa haina barabara ya lami lakini katika Serikali Awamu ya Tano, barabara imejengwa.
Katika kuonyesha kuwa jambo hilo limemfurahisha, mbunge huyo alipiga magoti, pembeni ya kiti anachoketi bungeni akimshukuru Rais Magufuli.
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Social Plugin