Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika amefunguka na kusema kuwa atawachukulia hatua watumishi wa serikali ambao wanazuia barua za watumishi wengine hasa walimu wanaotaka uhamisho zisimfikie yeye au Katibu au Waziri Mkuu.
Mkuchika amesema hayo bungeni na kudai kuwa yapo malalamiko ya baadhi ya walimu kushindwa kuhama kutokana na viongozi wao kuzuia barua zao zisifike kwake au viongozi wengine ambao wana mamlaka.
"Sasa naomba kulieleza bunge hili tukufu mwenye mamlaka ya kumkatalia uhamisho ni yule anaye andikiwa barua
"Wewe uliyeandikiwa pale kupitia kwa kiswahili sanifu kabisa, wakishasema kupitia kwa wewe si muamuzi wa mwisho, peleka barua kwa mwajiri ili mwajiri apate kuamua
"Mimi natembelea mikoani nimepata kupita mkoa mmoja naambiwa hii ofisi yetu haijapitishwa barua ya mtu kuhama hata moja, mimi nasema mimi ndiyo Waziri wa Utumishi wa Umma, nikimbaini kuna kiongozi wa utumishi anakataa kupitisha barua isinifikie mimi, isimfikie Katibu Mkuu Kilimo, isimfikie Waziri Mkuu nitamshughulikia mwa mujibu wa sheria na taratibu
"Nitafanya hivyo kwa sababu mtu huyo amejichukulia madaraka ambayo si yake, hukuandikiwa wewe barua halafu wewe ndiye unaamua sasa mimi niliyejuu nitafanya kazi gani kama wewe unaniamulia" alihoji Mkuchika
Mbali na hilo Mkuchika amesema kuwa zoezi la kuajiri sasa linatarajiwa kuendelea baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki kukaribia kukamilika na kusema serikali itaendelea na kutoa ajira mpya.
"Tutaendelea na ajira mpya kama nilivyosema 50,200 wa mwaka jana na mwaka ujao serikali imejipanga kuajiri 49,000" alisema Mkuchika
Social Plugin