Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy ambaye amepatwa na mkasa wa kuvuja kwa video yake ya faragha amefunguka na kusema kuwa kwa sasa ameamua kuacha kufanya kazi ya sanaa kwa muda mpaka atakapokuwa sawa ndiyo atarudi kufanya sanaa.
Nandy ameweka wazi hayo leo na kusema ni kweli yeye ndiye aliyerekodi video hiyo lakini hakuwa na lengo la kuivujisha bali alifanya hivyo kwa mapenzi yake lakini hausiki katika kuisambaza video hiyo.
"Kiukweli niko katika wakati mgumu wa maisha yangu.. jana sikuwa sawa ila leo nimeweza hata shika simu yangu najuaa matusi yote na fedheha kutoka kwa mashabiki wangu ni sababu wanaamini hili ni kusudio letu au langu hii video iwe public naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea. sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida! Sitakiwi kujieleza sana ila naamini nikiandika hili nitakaa na amani kwa ambaye ataamuaa kuendelea kuni hukumu aendelee tu kunihukumu kwani kweli nimekosea ila ajiulize kama yeye hajawahi kukosea! Mambo yetu wote ya private yanatakiwa kubaki private, aliyeyatoa amefanikiwa kuleta hii taharuki, sintofahamu na maumivu makubwa ambayo sijawahi kupata maishani mwangu"
Nandy aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo "ilaa naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!! nilibadili simu yangu mara 2 toka 2016 na Bilnas aliibiiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake, so hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani? maswali ni mengi matusi ni mengi simu na sms ni nyingi mnoo, sikatai nimerecord video na nilikuwa kwenye mahusiano na nilifanya kwa mapenzi ila siwez weka public, Mungu anisamehe kwa niliyowakwaza"
Kufuatia kadhia hiyo ambayo Nandy amekutana nayo video yake ya faragha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ameamua kukaa pembeni ya sanaa kwa muda na kusema pindi atakapokuwa sawa ataweza kurudi na kuendelea na sanaa.
"Nimepoteza watu wa maana nahisi ku poteza vitu vingi ilaa nashukuru sana kwa watu wangu wa karibu waliolia na mimi mashabiki wanaoniamini mimi na dhamira yangu ya kweli, marafiki walio liaa kwa ajili yangu nawashukuru sana mnoo yote naomba radhi sana sana kwa kilicho tokea haikuwa kusudio langu na naumiaa sana!!! asante sana BASATA kwa ushirikiano wenu kwakuwa na mimi na kunipa moyo hii ni fundisho kwa wote nimejifunza kitu kikubwa sana!! mashabiki, serikali yangu viongozi wenye imani na mimi, mashabiki zangu, ndugu jamaa na marafiki. naomba Nisameheni naamini na hili nalo litapita. Sitaongea tena kwenye vyombo vya habari kuhusu hili namwachia Mungu, pale roho yangu itakapopata wepesi tutaonana tena kwenye Sanaa. Naomba mniombee nipate wepesi wa kuvuka hili daraja" alisisitiza Nandy
Social Plugin