Baada ya kuvuja kwa video inayowaonyesha wanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na Billnas wakiwa faragha na ambayo imezua gumzo jan katika mitandao ya kijamii, Nandy amekiri kwamba video hiyo ni ya kweli japo ni ya mwaka 2016 na amewaomba msamaha Watanzania kwa walioiona video hiyo. Leo amefika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kujieleza na baada yakutoka kasema haya kupitia akaunti yake ya instagram;-
”Kiukweli niko katika wakati mgumu wa maisha yangu.. jana sikuwa sawa ila leo nimeweza hata shika simu yangu najuaa matusi yote na fedhea kutoka kwa mashabiki wangu ni sababu wanaamini hili ni kusudio letu au langu hii video iwe public naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea!!! sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida!
Sitakiwi kujieleza sana ila naamini nikiandika hili nitakaa na amani kwa ambaye ataamuaa kuendelea kuni hukumu aendelee tu kunihukumu kwani kweli nimekosea ila ajiulize kama yeye hajawahi kukosea! Mambo yetu wote ya private yanatakiwa kubaki private, aliyeyatoa amefanikiwa kuleta hii taharuki, sintofahamu na maumivu makubwa ambayo sijawahi kupata maishani mwangu. ilaa Naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!! nilibadili simu yangu mara 2 toka 2016 na bilnas aliibiiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake, so hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani? maswali ni mengi matusi ni mengi simu na sms ni nyingi mnoo… naumiaa naumiaa kupita kiasi.
Kanisaa langu, wazazi wangu, ndugu zangu, marafiki zangu wa karibu wameliaa sana sanaa mnoo!!! sikatai nimerecord video na nilikuwa kwenye mahusiano na nilifanya kwa mapenz ila siwez weka public, Mungu anisamehe kwa niliyowakwaza. nimepoteza watu wa maana nahisi ku poteza vitu vingi ilaa nashukuru sana kwa watu wangu wa karibu waliolia na mimi mashabiki wanaoniamini Mimi na dhamira yangu ya kweli, marafiki walio liaa kwa ajili yangu nawashukuru sana mnoo yote naomba radhi sana sanakwa kilicho tokea haikuwa kusudio langu na naumiaa sana!!! asante sana basata kwa ushirikiano wenu kwakuwa na mm na kunipa moyo hii ni fundisho kwa wote nimejifunza kitu kikubwa sana!! mashabiki, kabisa langu, serikali yangu viongozi wenye imani na mimi, mashabiki zangu, ndugu jamaa na marafiki. naomba Nisameheni naamini na hili nalo litapita. Sitaongea tena kwenye vyombo vya habari kuhusu hili namwachia Mungu, pale roho yangu itakapopata wepesi tutaonana tena kwenye Sanaa. Naomba mniombee nipate wepesi wa kuvuka hili daraja.🙏🏼”
Social Plugin