Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametangaza rasmi utaratibu mpya wa kuingia bungeni utakaotumiwa na Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge wakati wanapokuwa wanaingia na msafara na kudai utaratibu huo unaweza kuwasaidia kiusalama zaidi.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo mapema leo asubuhi wakati alipowasili Bungeni kwenye kikao cha nane, mkutano 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia mlango wa nyuma karibu na kiti chake ambacho anakikalia pindi anavyokuwa anaendesha shughuli za Bunge tofauti na ule mpangilio uliokuwa umezoeleka kuonekana kila uchao wa kupita kati kati ya Wabunge wote Bungeni.
"Utaratibu huu unafaida nyingi, wakati mwingine mnaweza mkawa na hasira tunapopita hapa katikati mkaturukia", amesema Ndugai
Spika Ndugai amesema ingawa haimo kwenye kanuni, lakini mabadiliko hayo yanafanyika ili kuendana na nchi nyingine zilizoendelea.
Aidha, Spika Ndugai amesema mlango mkuu wa kuingia Bungeni watautumia kupita endapo kutakuwa na ugeni wa kitaifa kama vile Rais na kufunga au kufungua Bunge na sio vinginevyo.
Social Plugin