Taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo leo April 9, 2018 ni kwamba kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufariki Mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari nchini humo ni kwamba Padri huyo Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.
Inafikiriwa kuwa muuaji huyo ni sehemu ya kikundi cha waasi cha Mai Mai Nyaturaambacho ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini ikiwa ni pamoja na kuiba mali za wanakijiji.
Social Plugin