Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya amefungua rasmi Hoteli ya Kisasa ya Lyakale “Lyakale Hotel” iliyopo katika mtaa wa Majengo Mapya kata ya Ngokolo mjini Shinyanga inayomilikiwa na Christopher Ringo.
Hafla fupi ya uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa imefanyika jana Jumamosi Aprili 14,2018 usiku na kuhudhuriwa na viongozi wa kiserikali,dini,siasa,wafanyabiashara na watu mbalimbali.
Awali Nkya aliongoza ibada ya kubariki jengo hilo litalotumika kutoa huduma bora za malazi,vyakula na vinywaji kwa wageni wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
“Mungu alitupa wajibu wa kufanya kazi,kufanya kazi siyo matokeo ya kufanya dhambi,ni wajibu ambao binadamu amepewa na Mungu….Na Mungu anatubariki kupitia kazi zetu,tunapofanya kazi tukimtegemea yeye Mungu na yeye anakuwa pamoja nasi,anaweka mkono wake anatuwezesha,hivyo mnaofanya kazi msifanye kwa akili zenu bali mfanye kwa kumtegemea mungu,naamini kwa kazi hii niliyoifungua mtakula matunda ya kazi hii maana mmemkabidhi Mungu”,aliongeza Nkya.
Akizungumza wa hafla hiyo,Mkurugenzi na Mmiliki wa Lyakale Hotel Christopher Ringo alimshukuru Mungu katika kufanikisha kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa hotel uliodumu kwa takribani miaka 10 na kuwaomba wadau mbalimbali kuunga mkono huduma zinazotolewa katika hoteli hiyo.
“Mchakato wa ujenzi umechukua muda mrefu,na ilifikia mahali tukaona tunachoka lakini kwa kuwa tulikuwa tunamtegemea Mungu tumefanikiwa,tunaamini kupitia mradi huu tutaweza kukuza pato la taifa kwa njia ya kodi na kutoa huduma bora za malazi,vinywaji na vyakula vya aina mbalimbali na kuhifadhi vyombo vya usafiri kwa wageni katika hali ya usalama”,alieleza Ringo.
“Pamoja na mradi huu kuwa chanzo cha kipato cha familia na jamii inayotuzunguka pia tutaboresha utoaji wa huduma za Kihoteli kwa kuongeza ushindani katika soko ili kuwanufaisha walaji na uwekezaji wa muda mrefu”,aliongeza Ringo.
Lyakale Hotel ipo mtaa wa Majengo Mapya katika kata ya Ngokolo mkabala na Malaika Hotel mjini Shinyanga, kwa mawasiliano zaidi piga simu namba +255 763260 982, +255 754 069 500 au kwa barua pepe lyakale@gmail.com
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa nje wa Lyakale Hotel iliyopo mjini Shinyanga- Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Bango katika Hotel ya Lyakale
Geti la Lyakale Hotel
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya akiongoza ibada ya kubariki jengo la Lyakale Hotel wakati wa hafla fupi ya ufunguzi rasmi wa hoteli hiyo jana usiku Aprili 14,2018
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya akiendelea na ibada wakati wa ufunguzi wa Lyakale Hotel
Mkurugenzi wa Lyakale Hotel, Christopher Ringo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufungua Lyakale Hotel . Kushoto ni mke wa Mkurugenzi wa Lyakale Hotel 'Mama Ringo'
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya akizungumza wakati wa kufungua Lyakale Hotel
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya akikata utepe kufungua rasmi Lyakale Hotel
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya akisoma neno la Mungu baada ya kukata utepe
Mchungaji Nkya akiingia katika Hoteli ya Lyakale
Mchungaji Nkya akiwa ndani ya Lyakale Hotel
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya akiendelea na ibada ndani ya jengo la Lyakale Hotel
Ibada ya kubariki na kuweka wakfu jengo la Lyakale Hotel ikiendelea
Mchungaji Nkya akiomba ndani ya Lyakale Hotel
Mchungaji Nkya akibariki moja ya vyumba katika jengo hilo
Muonekano wa moja ya vyumba katika Lyakale Hotel
Mchungaji Nkya akibariki chumba katika Hoteli ya Lyakale
Viongozi na wananchi mbalimbali wakiwa ndani ya Lyakale Hotel
Mchungaji Nkya akiendelea kubariki vyumba .Kushoto ni Mama Ringo akifuatiwa na mme wake Christopher Ringo
Mchungaji Nkya akibariki sehemu ya kulia chakula katika Lyakale Hotel
Mchungaji Nkya akiendelea kubariki sehemu ya kupikia chakula
Mchungaji Nkya akibariki vyoo vilivyopo katika hoteli hiyo
Mchungaji Nkya akiendelea kubariki maeneo mbalimbali ya Lyakale Hotel
Mkurugenzi wa Lyakale Hotel Christopher Ringo (Kulia) akimshukuru Mchungaji Nkya baada ya kubariki jengo la hoteli hiyo
Mzee Ringo akishikana mkono na Mchungaji Nkya
Muonekano wa moja ya vyumba katika hoteli ya Lyakale
Muonekano wa chumba chenye double
Muonekano wa sehemu ya bafu
Muonekano wa chumba kingine katika Lyakale Hotel
Sehemu ya kulia chakula 'Restaurant'
Mchungaji Nkya akichukua chakula,ikiwa ni sehemu ya hafla fupi ya uzinduzi wa Lyakale Hotel
Mapadri wa kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga wakichukua chakula
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akichukua chakula
Wageni waalikwa wakiendelea kuchukua chakula.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin