Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amezindua chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ‘Human Papilloma Virus Vaccine – HPV Vaccine' kwa ajili ya wasichana wenye umri wa miaka 14.
Akizungumza wakati wa kufungua chanjo hiyo leo Jumatatu Aprili 23,2018 katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga, Telack alisema lengo la chanjo hiyo ni kuwakinga wanawake dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kuanzia Mwezi Aprili,2018 nchi nzima.
Alisema uzinduzi huo umefanyika katika halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga na kwamba wiki ya chanjo kitaifa iliyoanza leo Aprili 23,2018 itaendelea hadi Aprili 29,2018 baada ya hapo chanjo itaendelea kutolewa kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali na binafsi na katika shule.
“Hii chanjo inatolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 tu na kauli mbiu ya chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi,Chanjo ya sindano ya Polio kwa watoto na wiki ya chanjo kwa ujumla ni ‘Jamii iliyopata chanjo ni jamii yenye afya,timiza wajibu wako”,alisema Telack.
Alibainisha kuwa walengwa wa chanjo hiyo ni wasichana wote waliotimiza miaka 14 ambapo wasichana 29,479 wanatarajiwa kuchanjwa ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani ya mlango wa kizazi.
Alisema saratani hiyo ndiyo ya kwanza kusababisha vifo vitokanavyo na saratani ikifuatiwa na saratani ya matiti hivyo juhudi na ushirikiano vinahitajika zaidi katika kupunguza vifo hivyo.
Aliongeza kuwa wakati wa chanjo hiyo pia panatolewa chanjo ya kuwakinga watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa njia ya sindano ‘Injectable Polio Vaccine – IPV.'
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizindua Chanjo mpya ya Kuzuia saratani ya mlango wa kizazi katika viwanja vya Zimamoto mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwasisitiza wasichana wenye umri wa miaka 14 kupata chanjo itakayowakinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akielezea namna wilaya yake ilivyojipanga kufanikisha chanjo mpya ya Kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ‘Human Papilloma Virus Vaccine – HPV Vaccine'.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume akielezea namna chanjo hiyo itakavyofanyika mkoani Shinyanga.
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo.
Mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Deogratius Maufi akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwakilishi kutoka Shirika la afya Duniani (WHO) Dkt. Gerald Maro akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Muuguzi kutoka Zahanati ya kanisa la KKKT Mjini Shinyanga Modesta Chitanda (aliyeshikilia kipaza sauti) akimweleza mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack (katikati) namna wanavyotoa huduma ya chanjo ya Kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ‘Human Papilloma Virus Vaccine – HPV Vaccine .Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifungua dawa ya chanjo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akionesha dawa ya chanjo
Muuguzi kutoka Zahanati ya kanisa la KKKT Mjini Shinyanga Modesta Chitanda akimuonyesha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack namna wanavyoweka dawa ya chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi
Muuguzi kutoka Zahanati ya kanisa la KKKT Mjini Shinyanga Modesta Chitanda akimpatia chanjo ya Saratani ya kinga ya mlango wa kizazi mwanafunzi Jesca Kashinje(14) kutoka shule ya Sekondari Mwasele iliyopo katika manispaa ya Shinyanga.
Mwanafunzi Jesca Kashinje(14) kutoka shule ya Sekondari Mwasele iliyopo katika manispaa ya Shinyanga akifurahia baada ya kupewa chanjo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akisikiliza maelezo katika banda linalotoa huduma ya upimaji malaria na VVU.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikisisitiza jambo katika banda hilo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitembelea banda linalotoa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na msafara wake wakiondoka kwenye mabanda.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali zilizopo katika manispaa ya Shinyanga wakiwa katika foleni kuelekea kwenye banda linalotoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi.
Wanafunzi wakiwa katika viwanja vya zimamoto mjini Shinyanga
Wadau mbalimbali wakiwa katika eneo la uzinduzi wa chanjo hiyo
Wadau wakiwa eneo la uzinduzi.
Kundi la burudani ya ngoma "Mabulo ya Jeshi' likitoa burudani.
Kwaya ya AICT Shinyanga wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya saratani ya mlango wa kizazi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akicheza wimbo maalumu kutoka kwaya ya AICT Shinyanga.
Wadau wakiwa eneo la uzinduzi.
Wadau wakiwa eneo la tukio
Wadau wakiwa eneo la tukio
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje akitoa neno la shukrani baada ya uzinduzi wa chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi katika mkoa wa Shinyanga
Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya akitoa neno la shukrani baada ya uzinduzi wa chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi katika mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
VIDEO VIGOGO WA SHINYANGA WAKICHEZA WIMBO MAALUM
VIDEO VIGOGO WA SHINYANGA WAKICHEZA WIMBO MAALUM
Social Plugin