Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo (kushoto0 na Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Zakia Meghji wakipia saluti salamu ya kiskauti baada ya Meghji kuvishwa beji na skafu wakati wa hafla iliyoandaliwa na TGGA kwa mwenyekiti huyo jana katika Makao Makuu ya TGGA, Upanga Dar es Salaam.
Rakotondratovo ambaye aliambatana na Meneja Mahusiano, Marie Rafenoarisoa alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo alitembelea Makao Makuu ya TGGA Upanga na miradi ya chama hiyo. Ziara hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuipongeza TGGA kwa kuwa wa kwanza Afrika kusajiri wanachama wengi wakifuatiwa na Kenya na Nigeria.
Mwenyekiti wa Afrika wa World Association
of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo akionesha zawadi ya kitenge alichozawadiwa na Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema wakati wa hafla hiyo ya kumuaga.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Grace Makenya akimvalisha khanga Meneja Mahusiano,Marie Rafenoarisoa
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Grace Makenya akimvalisha Rakotondratovo khanga baada ya zawadi hiyo kumkabidhi.
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symporosa Hangi (kushoto) na Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema (kulia0 wakitoka kumpokea Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo tayari kuingia kwenye hafla ya chakula cha usiku Makao Makuu ya TGGA, Upanga
Meghji akimlaki Meneja Mahusiano wa WAGGGS Afrika, Marie Rafenoarisoa
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symporosa Hangi akitoa utambulisho wa baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya TGGA, Grace Makenya akitambulishwa
Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akitambulishwa
Marafiki wa TGGA wakitambulishwa
Viongozi wa TGGA kutoka Mkoa wa Lindi wakitambulishwa
Girl Guides wakitambulishwa
Wafanyakazi wa TGGA Makao Makuu, wakitambulishwa
Saada El Maamry akimtuza msanii
Msanii aliyekuwa akitumbuiza katika hafla hiyo akituzwa na Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi na Rafiki wa chama hichoClara Makenya.(kulia)
Rakotondratovo akipata mlo wa usiku ulioandaliwa kwa ajili yake wakati wa hafla ya kumuaga
Kamishna wa Kimataifa wa TGGA, Miryam Mjema akiwa na marafiki wa chama hicho Mecy Mchechu na Saada El-Maamry walipokuwa wakichukua mlo wa usiku
Sasa ni wakati wa maakuli
Wakicheza muziki
Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo (kushoto), akimvisha beji Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Abdallah ikiwa ni shukrani baada ya mbunge huyo kutoka Mkoa wa Lindi kuhudhuria hafla hiyo
Mwenyekiti wa Afrika wa World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), Zoe Rakotondratovo akitoa neno la shukrani
Viongozi wa TGGA wakiwa na marafiki wa chama hicho
Viongozi wa TGGA, wakiwa na wafanyakazi wa TGGA Makao Makuu
Mjumbe wa Kamati ya WAGGGS Afrika, Florentina Mganga akimvisha zawadi ya skafu Zakia Meghji
Meghji akivishwa beji ya WAGGGS
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0754264203
Social Plugin