Wananchi wanaokadiriwa kuwa 400 wamevamia eneo la pembezoni mwa mgodi wa Acacia Bulyanhulu katika kijiji cha Namba tisa kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa Shinyanga kwa lengo la kuchimba mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya dhahabu.
Wananchi hao wamevamia eneo hilo jana Jumanne Aprili 10,2018 majira ya saa nne na nusu asubuhi.
Inaelezwa kuwa eneo lililovamiwa bado haijathibitishwa kuwa nani ni mmiliki halali kwani mgodi wanadai wana leseni ya eneo hilo huku Mayunga Peter ambaye ni mkulima wa kijiji hicho cha namba tisa akidai kuwa hilo ni eneo lake kwani hajalipwa fidia na mgodi.
Kufuatia mgogoro huo,Malunde1 blog imeelezwa kuwa viongozi wa jeshi la polisi halmashauri ya Msalala pamoja na viongozi wa kijiji na kata walifika eneo husika kuangalia hali halisi ya usalama wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kufanya kikao kati ya uongozi na serikali ya kijiji , uongozi wa mgodi pamoja na jeshi la polisi na kwamba hali ya usalama imeimarika hakuna uvunjifu wa amani.
Malunde1 blog inaendelea kumtafuta Mkuu wa wilaya ya Kahama ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo,Fadhili Nkurlu ili kuzungumzia mgogoro na kuelezwa kuwa yupo kwenye kikao cha usuluhishi kati ya wanakijiji na uongozi wa mgodi wa Bulyanhulu.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Zainab Telack amesema amepokea taarifa kuhusu mgogoro huo na kwamba serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Wananchi wakiwa katika eneo linalodaiwa kuwa na madini ya dhahabu pembezoni mwa mgodi wa Bulyanhulu
Mwananchi akiwa ndani ya shimo akisaka dhahabu
Wananchi wakiwa katika eneo linalodaiwa kuwa na mchanga wenye madini ya dhahabu pembezoni mwa mgodi wa Bulyanhulu
Viongozi wa jeshi la polisi na mgodi wa Bulyanhulu wakiwa katika eneo hilo
Wananchi wakiwa eneo linalodaiwa kuwa na madini ya dhahabu
Askari polisi wakiwa eneo hilo
Askari polisi wakiwa katika eneo hilo
Social Plugin