Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda jana April 9 amezungumza na akina mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.
Ambapo alieleza maumivu na masimango ya peke yao yamekoma sasa ni mguu kwa mguu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Makonda alisema kuwa mchakato huo utafanyika kwa siku tano na wasaidizi wake wa huduma za sheria watahudumia kwa haki.
Alieleza hawapo kwa ajili ya kumkomoa mtu ila ni kulinda haki za Mama na mtoto na kama baba wa watoto hao hawatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.
"Kama tukikuita hutaki, unajificha unajidai kulinda ndoa yako wakati mama yangu huku anateseka na mtoto huku sisi tutakuanika hadharani mkeo ajue una mtoto wa nje ya ndoa
"Mimi najua sijaanza leo kupigana hii vita najua wakina baba wasiopenda matokeo yao watanichukia lakini ukinichukia, ukinitukana, kunifedhehesha ni kama unanipaka mafuta yanayoning'arisha zaidi chuma kinaimarishwa na moto na viongozi wanaimarishwa na kebehi" alisisitiza Paul Makonda
Alisema Makonda ameeleza wakiona sheria haitoshi watapambana hadi Bungeni kubadili sheria ili kila mwanamke wa kitanzania apewe haki zake pamoja na mtoto na kuwe na usawa.
Aliwataka akina Mama waliozalishwa na wanaume wa kada zote kama walimu, wanasiasa, walio katika mabenki na kokote Tanzania watatafutwa popote ili kulinda haki za watoto na mama zao.
Makonda alieleza Serikali Rais Magufuli imewapa kazi ya kuwasikiliza wananchi na hivyo hawapaswi kukaa na madukuduku yao, hivyo walete malalamiko yao kwani watoto wanategemewa kwa mustakabali wa taifa la kesho.
Pamoja na hayo RC Makonda amewataka pia Wanaume walioachiwa watoto wafike ofisini kwake ili wapatiwe msaada wa kisheria.
Social Plugin