Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAOSHIRIKI MASHINDANO YA UREMBO TANZANIA KUAJIRIWA SHIRIKA LA NDEGE LA TAIFA

Waziri wa Habari , Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe amependekeza kuwa wanaoshiriki mashindano ya urembo wa ma-miss waajiriwe katika shirika la ndege la taifa kwa sababu wana vigezo vya kutosha.

Mh Harrison Mwakyembe aliyasema hyo katika uzinduzi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 yatakayofanyika chini ya kampuni ya The Look baada ya ile ya Lino kuachia ngazi hiyo.


Mh Waziri amesema kuwa washiriki wengi wa mashindano hayo wanakuwa na uwezo na sifa nyingi za kuwa katka cabin crew ila tu kabla ya kuajiriwa wanapaswa kupelekwa kozi fupi ya miezi mitatu katika chuo cha anga kabla ya kuanza kazi na hii itapunguza tatizo la ajira kwa warembo hao.


Hii pia inaweza kusaidia baadhi ya wasichana kwa sababu kuna warembo wamekuwa wakishiriki mashindano hayo na baadae dira zao za maisha kupotea na kujikuta wakiishi maisha magumu sana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com