Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MHAGAMA AWAGEUKIA VIONGOZI WA DINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama amewageukia viongozi wa dini mbalimbali na kuwasii waendelea kuliombea taifa ili iweze kudumishwa amani na utulivu huku akiwapongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kufanya hivyo.


Waziri Mhagama anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu nchini ametoa pongezi hizo alipokutana na uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.


"Niwapongeze sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo", amesema Waziri Mhagama.


Aidha, Waziri Mhagama amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wa dini na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt.John Magufuli katika kufikia azma yake ya "Tanzania ya Viwanda".


"Kipekee niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu uongozi wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na viongozi wote kwa ujumla wao, ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo", amesisitiza Waziri Mhagama.


Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase akifanya maombi kwa kifupi walipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama kuzungumza masuala yao na kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada za kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla.


Pamoja na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika huduma za kijamii hususani kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na shule, vyuo na zahanati zinazohudumia wananchi wanaochangia katika uzalishaji na maendeleo ya nchi yao.


kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com