
Alikiba alitoa ahadi hiyo mnamo Mei 2, 2018 kupitia mtandao wake wa kijamii instagram mara baada ya Ommy Dimpoz kuachia ngoma yake ya 'Yanje' aliyomshirikisha Seyi Shay kutoka Nigeria licha ya video hiyo kutofikisha watazamaji milioni 3 kama alivyotaka iwe.
Wimbo huu, Alikiba ndio wa kwanza kuachia tangu alipoingia katika ulimwengu mpya wa ndoa siku za hivi karibuni huku mashabiki zake wakimpongeza msanii huyo kwa kuweza kubadilika badilika kila anapoamua kurudi tena katika muziki.
Kama hujapata bahati ya kutazama video mpya ya Alikiba tazama hapa chini.
Social Plugin