Takribani watu 22 wakiwemo watoto watatu wamefariki kwenye ajali ya basi kaskazini mwa Uganda kwa mujibu wa polisi.
Basi hilo liligonga tingatinga ambayo ilikuwa ikiendeshwa bila ya taa usiku kwa mujibu wa msemaji wa polisi Emilian Kayima ambaye aliongea na AFP.
Ajali hiyo ilitokea Ijumaa usiku huko Kiryandongo karibu kilomita 220 kaskazini mwa mji mkuu Kampala.
Baadhi ya vyombo vya habari vilisema kuwa watu waliofariki dunia walikuwa zaidi ya 30.
Uganda ina kati ya rekodi mbaya zaidi za usalama wa barabara. Zaidi ya watu 9,500 walifariki kwenye ajali za barabarani nchini humo kati ya mwaka 2015 na 2017 kwa mujibu wa takwimu rasmi.
Chanzo- BBC
Social Plugin