BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA JIJINI ARUSHA


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha leo ,kuhusu mkutano mkuu wa ishirini na tatu wa Wanahisa unaotarajia kuanza rasmi Mei 18,2018 na kumalizika Mei 19,2018 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC uliopo jijini Arusha.
Kudhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei kulia ni Mkurugenzi wa mikopo James Mabula. 
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa masoko wa CRDB Jadi Ngwale,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei
Waandishi wa habari wakiwa wanafanya mahojiano ya kina kuhusu mkutano huo - Picha zote na Pamela Mollel,Arusha
***
Benki ya CRDB inatarajia kufanya mkutano wake wa ishirini na tatu(23)wa wanahisa wa benki hiyo katika ukumbi wa Kimataifa wa AICC uliopo jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei alisema kuwa mkutano huo wa wanahisa unatarajiwa kufanyika Mei 19,2018 na  kuhudhuriwa na watu zaidi ya elfu moja .

Dkt.Kimei alisema kuwa Mkutano huo wa wanahisa wa benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalumu kwa wanahisa wa benki hiyo utakaofanyika tarehe 18 mwezi huu ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa watapata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali kibenki.

Alisema kuwa agenda za mkutano huo ni kupokea na kupitisha taarifa za fedha na ripoti za wakurugenzi kwa mwaka uliopita tarehe 31 mwezi Disemba 2017,kuidhinisha taarifa maalumu ya gawiyo wa mwaka ,kuchagua wajumbe wa bodi ,kuhidhinisha
uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaokupalika kisheria.

Dkt Kimei alitoa rai kwa wanahisa wa benki hiyo kuuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo mkuu huku akiongeza kuwa kwa mwanahisa ambaye hataweza kuudhuria anahaki ya kuchagua mwakilishi au wawakilishi kuudhuria na kupiga kura kwa niaba yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post